" Mafanikio daima ni kwa wale wenye Kujaribu bila kujali mara ngapi wanaanguka "

 

 

 
Wednesday, May 25, 2005

Hivi kweli hawa ni watumishi wa mungu au waigizaji?

Hivi ni kweli siku hizi kuna dini kweli au ndio kusema siku za mwisho zimekaribia hivyo manabii wa uongo wanajitokeza na kupotosha watu kama alivyofanya padre huyu hapa.

Thursday, May 19, 2005

Kwa kweli hili linahitaji maombi pia!

Tulikuwa tumeanza kusahau lakini inavyoonyesha tabia hii ya kuchuna ngozi binadamu imerudi tena kwa kasi na kufanya watu mbalimbali kuzungumzia jambo hili kama anavyoelezea Askofu.soma hapa.

Tuesday, May 17, 2005

Tushirikiane katika kutunza familia!

Huyu nae alikuwa anamaanisha kuwa kama ni haki sawa basi hata wewe Mama nae una haki ya kutunza familia kwa kutukuchangia kipato katika familia yako. soma hapa.

Saturday, May 07, 2005

Urembo waelekea kuikomboa Tanzania

Kwa wale ambao wamekuwa wakiendelea kuwa na mawazo kuwa fani ya Urembo, Mavazi na Mitindo kuwa ni ya kumdhalilisha Mtanzania, au Mwafrika kwa ujumla kama ambavyo baadhi yetu tumekuwa tukilazimishwa kuamini, bilashaka watatakiwa kusoma hapa, kwanza kabla ya kuanza kutetea au kukanusha hoja yao hiyo.

Friday, May 06, 2005

Maoni ya wanawake kuhusu kikwete!

Wanawake wengi wameonekana kuupokea kwa shagwe sana uteuzi wa Waziri kikwete kugombea urais kwa kupitia CCM huku wengine wakidai kuwa ni mkombozi wao na kusahau kuwa ukombozi wao utaletwa na wao wenyewe na si vinginevyo.

Wapo waliosikika wakisema kuwa "sasa tumeula" wakimaanisha sasa maisha yao yatakwenda kama walivyopananga kwani kikwete aliwaahidi nini kina mama ambacho Marais waliopita walishindwa kutekeleza? Mimi sijui.

Wengine walisikika wakisema kuwa ana huruma sana na akinamama na kuwa siku zote amekuwa akiwatakia mema, wapo waliosema kuwa sasa kazi nje nje wakimaanisha kuwa watapata ajira bila wasi wasi.Mimi Binafsi siku zote napenda Kiongozi atakayeniwekea mazingira mazuri ya kuweza kufanya kazi na kupanga maisha yangu kama ndoto zangu.

Na mwenye kumthamini, kumheshimu na kumjali mwanamke yeyote ambaye yupo katika dunia hii bila kujali anakaa wapi, amezaliwa katika familia gani,ni mke au mtoto wa nani, ila awaone wote ni sawa kwake.

Wednesday, May 04, 2005

Mambo yanazidi kuiva, Ni kiswahili kwenda mbele sasa

Kiswahili, kiswahili kiswahili. Yaani ni kiswahili kwenda mbele hivi sasa. Hivi karibuni nimepokea na kupata anwani mpya za wanablogi wanaotumia lugha ya Kiswahili, ambazo ni pamoja na ya Martha Mtangoo na Beatrice Daffa, wanaoblogi kutokea Dodoma Tanzania na nyingine ya Indya Nkya, ambaye yeye yuko Moshi (Kilimanjaro) pia Tanzania.

Ndugu zangu, Watanzania wenzangu na wanablogi wenzangu, nina jambo moja ambalo napenda mlichukue kama neno langu la kuwakaribisha. Wakati nilipokuwa naanza kublogi kwa mara ya kwanza kabisa, sikuwa hata najua nini ninachokifanya, lakini kwa kadiri ambavyo nimekuwa nikiendelea nimekuwa nikibaini kuwa kumbe sikuwa napoteza muda wangu bure. Kuna mambo mengi ambayo yatakuja mbele yetu na hakika hatutajuta kupoteza muda wetu, kwa mujibu wa kaka yangu Ndesanjo. Karibuni wandugu wapendwa

Tuesday, May 03, 2005

Hayawi hayawi, hatimae...........

Kuna msemo wa kale, wa Wahenga usemao, Hayawi hayawi, hatimaye huwa. Hili ndilo linalowatokea baadhi ya wazee wetu ambao walistaafu kutoka katika lililokuwa Shirikisho la nchi za Afrika Mashariki miaka kibao iliyopita lakini hadi leo hii hawajapewa mafao yao, ikiwa ni zaidi ya miaka 30 sasa. Lakini baada ya miaka yote hiyo, hatimaye kaibuka jamaa mmoja na kuwaahidi kuwa mafao hayo yako mbioni kuelekea mifukoni mwao hivi karibuni. Ni nani aliahidi hayo? Soma hapa

Monday, May 02, 2005

Wanawake Tanzania wataka mabadiliko ya katiba

Ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, mwaka huu wa 2005, huenda ,mwanamke wa Kitanzania, akaendelea kusonga mbele katika jitihada zake za kujikomboa kutoka makucha ya uonevu, ukandamizwaji na udhalilishwaji. hatua hii itakuja ikiwa mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa na wanawake yatapitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, wajua mabadiliko hayo yamezungumzia nini au kugusia sehemu gani muhimu? Soma hapa

Wakombozi wa wanawake

Je wewe ni mwanamke na unahitaji msaada wowote kwa ajili ya masuala mbalimbali yatokanayo na imani potofu dhidi ya wanawake? Usipate shida, soma hapa kujua wapi pa kukimbilia ikiwa unahisi bado uko katika makucha ya ukandamizaji dhidi ya wanawake.

Kwanini wanawake tusishinde?

Hakika saa ya ukombozi wa mwanamke inazidi na itazidi kupamba moto kwa kwa nia ya kumkomboa mwanamke huyu ambaye alionekana kujengwa na kunyanyapaliwa na jamii kijinsia.

Miongoni mwa mambo ambayo yalikuwa sio tu yakimuumiza mwanamke, bali pia kumshushia hadhi yake ni pamoja na suala la Ukeketaji, mila ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikifanywa na makabila mbalimbali nchini Tanzania, kutokana na imani ambazo hakika zilikuwa zimelenga katika kumdhalilisha mwanamke.

Ni wazi kuwa mapambano ya kumkomboa mwanamke kutoka katika makucha ya mila potofu za kumkandamiza, kumdhalilisha na hata kumshushia thamani, lakini kwa juhudi za pamoja, nina imani kuwa hakuna wa kuweza kutuzuia kuweza kufikia malengo yetu.

Soma hapa kujua jinsi ambavyo baadhi ya wadau wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kuwasaidia wanawake kujikomboa kutoka katika makucha ya mila hii potofu.

KUHUSU MIMI

JINA:Zainab Yusuph
MAKAZI:Dodoma
NCHI:Tanzania
KAZI:Mwandishi

BLOGI ZA KISWAHILI

 • Bangaiza
 • Mwandani
 • Pambazuko
 • Damija
 • Mtafiti
 • Martha
 • Gaphiz
 • Swahili time
 • Miruko
 • Dira yangu
 • Msangimdogo
 • Jeff Msangi
 • Kasri la mwanazuoni
 • Kurunzi
 • Baragumu
 • Mawazohuru
 • Fikra Thabiti
 • Mtandaoni
 • Motowaka
 • Mkwinda
 • Ngurumo
 • Nyembo
 • Bwaya
 • Omega
 • Tafakari za Maisha
 • Nuru akilini
 • Mtandawazi
 • Mhujumu
 • Vijimamboz
 • Wakati wa Ukombozi
 • Kijiwe Joto
 • Watoto Wetu
 • Jungu kuu
 • Kisima cha Weledi
 • Jarida la Ughaibuni
 • Bhalezee
 • Sauti ya Baragumu
 • Kona yangu
 • Furahia Maisha
 • Bakanja
 • Terrie Swai
 • Fatma Karama
 • Kazonta
 • Binti Afrika
 • Blogu ya Kilimo
 • Ukombozi
 • Mwafrika
 • Digital Africa
 • Blogu ya lugha mseto
 • BLOGI ZA WAAFRIKA

 • BLOGAFRICA
 • BLOGU ZA WAAFRIKA
 • DIGITAL AFRICA
 • MAMA JUNKYARD'S
 • MSHAIRI
 • KENYAN PUNDIT
 • MONGI DREAMS
 • ISARIA MWENDE
 • CUNNING LINGUISTICA
 • ETHIOPUNDIT
 • MOCHALICIOUS
 • UNGANISHA
 • DEMOKRASIA KENYA
 • CHANUKA
 • BANKELE
 • MAARIFA/AKIEY
 • AFROMUSING
 • NEHANDA DREAMS
 • BLACK LOOKS
 • YUMMY WAKAME
 • AFRICAN OIL POLITICS
 • NUBIAN SOUL
 • SANAA
 • VIRTUAL INSANITY
 • MENTAL ACROBATICS
 • KENYA UNLIMITED
 • JIKUMBUSHE KAZI ZANGU ZA ZAMANI

  2005-04 2005-05 2005-06 2005-07 2005-08 2005-11 2006-05 2006-06

  Imetengenezwa na

  Bonyeza hapa kumtembelea msangimdogo

  na inawezeshwa na