" Mafanikio daima ni kwa wale wenye Kujaribu bila kujali mara ngapi wanaanguka "

 

 

 
Saturday, April 30, 2005

Juhudi za dhati za wanawake

Mmoja kati ya wana-Blogi wa kiswahili (Bw. Ramadhani Msangi), katika makala yake moja ametamka maneno haya:- "Amka mwanamke wa Kitanzania, amka mwanamke wa Kiafrika. Popote pale ulipo katika dunia hii, amka SAA YA UKOMBOZI NI SASA". wakati akiuelezea mkutano wa kwanza na wa aina yake kuwahi kufanyika ambao utawahusu akina mama toka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine, nafasi na ushiriki wao katika ulimwengu wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano, kwa njia ya mtandao wa kompyuta.

Katika siku za karibuni, nitaendelea kuwataarifu zaidi juu ya kile kitakachokuwa kikiendelea wakati tukiuelekea mkutano huo unaokwenda kwa jina la Blogher utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu, nchini Marekani. Wakati tukiwa tunasubiri kujua kitakachotokea huko, wale ambao watahitaji kujua kuwa maandalizi yanakwenda vipi kwa lugha ya kingereza wanaweza pia kufuatilia kwa kusoma hapa.

Ni bahati nzuri pia kuwa huenda mambo yakiwa kama yanavyoandaliwa, atakuwepo au watakuwepo Watanzania watakaoshiriki mkutano huo kwa minajili ya kuuripoti kwa njia ya mtandao mkutano huo, katika lugha ya kiswahili. Fuatilia juu ya hili kwa kubonyeza hapa.

Thursday, April 28, 2005

Tujirekebishe

Mimi huwa sishangai mtu anaposema kuwa anakunywa pombe kwa starehe bali nashangaa pale anapokunywa hizo pombe na baada ya kumaliza huporomosha matusi makubwa bila kujali kuwa wapo watoto ambao wangehitaji kuiga mema kutoka kwake.

Tabia hii kwa kweli sio nzuri na ningeomba wenye nayo wajirekebishe kwani haitajenga mazingira mazuri kwa watoto wetu hasa wale ambao siku zote wanaiga kutoka kwa wazazi au walezi wao na bila ya kubagua mambo ya kuiga wakidhani kuwa yote wanayoiga ni mema.

Ni kweli pombe ukinywa lazima utukane au utoe maneno machafu tena mbele ya watoto? mimi sidhani hilo lina ukweli hata kidogo kwani kama ingekuwa hivyo basi nchi hii ingejaa watu wasio na busara hata kidogo na ambao hawaheshimiki kwani suala la kutukana hadharani linashusha heshima ya mtu.

Kwani kama mtu atakuwa na mazoea ya kuwa kila atakapokunywa pombe ni lazima atoe matusi nina hakika hata kama ulikuwa unaheshimika kwa kiasi gani na watu wa hadhi gani? ni lazima heshima hiyo itapungua tena kwa kiasi kikubwa kwani matusi sio kitu cha kumuongezea mtu sifa bali kumdhalilisha tu.

Siku zote mimi naamini kila kitu kinawezekana kama mtu kweli atakuwa amedhamiria kukifanya kwa kuona umuhimu wake na madhara yake hivyo na hata hili la kubadilisha tabia za kutukana hadharani pia linawezekana.Na kama Mtu binafsi hawezi kunywa pombe bila kutukana basi ni vizuri akaacha kunywa hizo pombe na kubaki akiheshimiwa.

Wasomaji wangu msione labda mimi naingilia maisha ya watu bali haya ni kati ya yale mambo nisiyoyapenda mimi na kama kuna mwingine yanamkera. Naomba watu wasijenge chuki kwani kila mtu anacho anachokichukia hapa duniani.

Naomba mungu awabariki katika maisha yenu na shughuli zenu kwa ujumla.

Kwaherini na mkae salama.

Saturday, April 23, 2005

Unyama huu mpaka lini?

Kipigo,matusi,unyanyasaji wa kijinsia na mengime mengi machafu na ya kinyama yamekuwa yakizidi kutokea na kumfanya mwanamke aonekane bado hana haki katika jamii.

Mimi kama Mwanamke ambaye naamini mkombozi wa mwanamke ni mwamnamke mwenyewe nimekuwa nikijisikia vibaya sana kuzidi kuendelea kwa vitendo hivi vya kinyama dhidi yetu tena hasa vikiwa vimefanya na wanaume.

Hivi karibuni kumetokea kitendo kimoja cha kibaya sana dhidi ya Mwanamke ambacho mimi ninakiita ni cha kinyama kwani hastaili kufanyiwa binadamu wa aina yoyote yule hta kama nagekuwa amefanya kosa kubwa kiasi gani.

Tukio hilo ambalo lilitangazwa na vyombo vyetu vya habari hapa nchini
kuhusu Kijana mmoja ambaye aliamua kumnyanyasa Binti mmoja kwa kumuunguza na pasi ya umeme katika baadhi ya sehemu za mwili wake kwa kile alichokiita yeye kumkomesha.

Kijana huyo aliamua kufanya hivyo baada ya kunyimwa kufanya tendo la noa na binti huyo ambaye alikuwa akiamini kuwa yule ni kama kaka yake hivyo asingeweza kufanya nae kitendo hicho.

Mimi nikiwa kama mwanamke ambaye Nisingependa kuona vitendo hivyo vikiendelea kutendeka dhidi yetu napenda kuwaomba wanawake wenzangu ambao wako katika ngazi ya juu na wenye uwezo wa kumtetea mwanamke na wakasikika wawe mstari wa mbele katika kukemea hilo mwani mkombozi wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.

Mimi naamini uwezo tunao wa kujikomboa sisi wenyewe na kukemea kabisa vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikifanya dhidi yetu kwani hakuna atakayekuja kutukomboa bali ni sisi wenyewe tukiamua kupambana na wale wote ambao wanapenda kumkandamiza mwanamke.

Nawatakia Mapambano mema katika kumkomboa Mwanamke.

Wednesday, April 20, 2005

Nawashukuru Sana

Nawashukuru wote ambao wamejitokeza kunikaribisha katika uwanja huu. Bado niko katika maandalizi ya kuanza kuwasilisha maoni yangu kupitia safu hii na kuwapa nyie nafasi ya kuchangia. Ahsanteni na endeleeni kukaa mkao wa kula.

Friday, April 15, 2005

Ninabisha hodi

Inawezekana kabisa kuwa sina uzoefu wa kiasi hicho lakini kwakuwa siku zote nimekuwa nikiamini kuwa kujaribu ndio kufanikiwa, sikuona kwanini nami nisijiunge katika uwanja huu wa kubadilishana uzoefu kupitia njia ya Mtandao.

Kwa ujumla kuna watu wengi sana ambao wameniwezesha walau kufikia hatua hii na ambao naamini kwamba wataendelea kunipa msaada wa aina yoyote kuhusiana na mambo ya blogu, pindi nikiuhitaji kutoka kwao.

Kama niulivyokwisha sema awali, walo wengi lakini labda napenda kumshukuru Bw. Ramadhani Msangi, kwa niaba yao wote, namshukru sana kwa yote anayonifanyia na namuombea Mungu amjaalie maisha mema na marefu.

KUHUSU MIMI

JINA:Zainab Yusuph
MAKAZI:Dodoma
NCHI:Tanzania
KAZI:Mwandishi

BLOGI ZA KISWAHILI

 • Bangaiza
 • Mwandani
 • Pambazuko
 • Damija
 • Mtafiti
 • Martha
 • Gaphiz
 • Swahili time
 • Miruko
 • Dira yangu
 • Msangimdogo
 • Jeff Msangi
 • Kasri la mwanazuoni
 • Kurunzi
 • Baragumu
 • Mawazohuru
 • Fikra Thabiti
 • Mtandaoni
 • Motowaka
 • Mkwinda
 • Ngurumo
 • Nyembo
 • Bwaya
 • Omega
 • Tafakari za Maisha
 • Nuru akilini
 • Mtandawazi
 • Mhujumu
 • Vijimamboz
 • Wakati wa Ukombozi
 • Kijiwe Joto
 • Watoto Wetu
 • Jungu kuu
 • Kisima cha Weledi
 • Jarida la Ughaibuni
 • Bhalezee
 • Sauti ya Baragumu
 • Kona yangu
 • Furahia Maisha
 • Bakanja
 • Terrie Swai
 • Fatma Karama
 • Kazonta
 • Binti Afrika
 • Blogu ya Kilimo
 • Ukombozi
 • Mwafrika
 • Digital Africa
 • Blogu ya lugha mseto
 • BLOGI ZA WAAFRIKA

 • BLOGAFRICA
 • BLOGU ZA WAAFRIKA
 • DIGITAL AFRICA
 • MAMA JUNKYARD'S
 • MSHAIRI
 • KENYAN PUNDIT
 • MONGI DREAMS
 • ISARIA MWENDE
 • CUNNING LINGUISTICA
 • ETHIOPUNDIT
 • MOCHALICIOUS
 • UNGANISHA
 • DEMOKRASIA KENYA
 • CHANUKA
 • BANKELE
 • MAARIFA/AKIEY
 • AFROMUSING
 • NEHANDA DREAMS
 • BLACK LOOKS
 • YUMMY WAKAME
 • AFRICAN OIL POLITICS
 • NUBIAN SOUL
 • SANAA
 • VIRTUAL INSANITY
 • MENTAL ACROBATICS
 • KENYA UNLIMITED
 • JIKUMBUSHE KAZI ZANGU ZA ZAMANI

  2005-04 2005-05 2005-06 2005-07 2005-08 2005-11 2006-05 2006-06

  Imetengenezwa na

  Bonyeza hapa kumtembelea msangimdogo

  na inawezeshwa na