Pamoja na juhudi za Serikali za kujaribu kuondoa tatizo la njaa, tatizo hilo limeonekana kutaka kuota mizizi huku likisaidiwa na tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta.
Tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta limekuja wakati mbaya ambapo bado kuna tatizo la upungufu mkubwa wa chakula.
Huko masokoni chakula kilichopo hakitoshi, lakini kimepanda bei kutokana na gharama za usafirishaji kupanda. wakati ukirudi nyuma unakuja kukwama pale pale kwenye kupanda kwa bei ya mafuta.
Kumbe basi hili nalo ni tatizo tena kubwa ambalo linaweza kuleta madhara kama halitachukuliwa hatua mapema.
Baadhi ya madhara hayo tumeshaanza kuyaona ikiwa ni pamoja na kupanda kwa nauli za daladala na mabasi na kusababisha watu kushindwa kumudu hali ya gharama hizo na kuleta usumbufu mkubwa. kwani usafiri ni muhimu kwao sasa kama utakuwa wa gharama hilo si tatizo kubwa?
Nawatakia siku njema.