Wamarekani Wanatutafuta nini?
Inashangaza sana kuona kuwa eti kati ya watu, asasi na mashirika mbalimbali yaliyokuwa mashuhuda wa Uchaguzi uliofanyika kule katika Visiwa vya Zanzibar na kushuhudia Karume (yule mdogo) akirejea tena madarakani, ni Wamarekani tu ambao wameona kuwa Uchaguzi huo haukuwa sahihi. Lakini afadhali mambo yangeishia hapo kwa wao kutoa maoni yao tu kwa walivyouona...kufikia hatua ya kudai eti haukuwa halali na kutaka matokeo yake yabatilishwe??? Wamarekani ni akina nani kwa Watanzania?