Hivi ni kweli misaada ya mikopo iyasaidia kuondoa umaskini?
Pamoja na watu kuzungumzia suala hili kwa kirefu zaidi huku asilimia kubwa wakiamini kuwa ni kweli fedha wanazokopeshwanchi zinazoendelea na benki ya dunia zitasaidia kuondoa umaskini.Wapo ambao wamekuwa wakijiuliza kuwa ni muda gani sasa umepita tangu tumeanza kukopesha na bado hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya na yakusikitisha,mimi nikiwa mmoja wao.
Kwa kweli mpango huu mimi naona ni wa kuwafaidisha wachache na haswa wale ambao eti wamekuwa wakijidai kutukopesha kwa kigezo cha kutusaidia kujikwamua na na umaskini.
Hivi kuna maendeleo gani iwapo watatukopesha kwa vigezo vya kuwabinafsishia vitega uchumi vyetu,ambavyo ndio njia pekee ya kuweza kutupatia maendeleo? badala ya kutupatia elimu ya namna ya kuvitumia ili kujiletea maendeleo.
Kwakweli suala hilo mimi "Mbado" siliafiki kwa wao kuendelea kutukopesha huku wakituzulumu,ni bora "Umaskini wa mali kuliko wa akili'' nikimaanisha kuwa mali tunazo ila elimu ndio hatuna, hiuvyo hilo ndilo tunalohitaji.
Hii sio kampeni ya kuondoa umaskini, bali ya kuchochea umaskini!
Nawatakia kazi njema.