naomba kusaidiwa!
Jambo hili limekuwa likinitatiza sana na hatimaye nikibaki bila kuwa na jibu la uhakika kuwa kiwango cha uzee wa mtu kinapimwa na umri au maumbile{ nikimaanisha miondoko, mikunjamano ya uso pamoja na ya mwili}
Kwani hata watu wengi nimekuwa nikiwasikia wakijiuliza swali hilohilo bila kupata jibu na mwisho kila mmoja kutafsiri uzee vile ajuavyo yeye hivyo wapendwa wasomaji wa blogu yangu naomba mnisaidie.