Hakika saa ya ukombozi wa mwanamke inazidi na itazidi kupamba moto kwa kwa nia ya kumkomboa mwanamke huyu ambaye alionekana kujengwa na kunyanyapaliwa na jamii kijinsia.
Miongoni mwa mambo ambayo yalikuwa sio tu yakimuumiza mwanamke, bali pia kumshushia hadhi yake ni pamoja na suala la
Ukeketaji, mila ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikifanywa na makabila mbalimbali nchini Tanzania, kutokana na imani ambazo hakika zilikuwa zimelenga katika kumdhalilisha mwanamke.
Ni wazi kuwa mapambano ya kumkomboa mwanamke kutoka katika makucha ya mila potofu za kumkandamiza, kumdhalilisha na hata kumshushia thamani, lakini kwa juhudi za pamoja, nina imani kuwa hakuna wa kuweza kutuzuia kuweza kufikia malengo yetu.
Soma
hapa kujua jinsi ambavyo baadhi ya wadau wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kuwasaidia wanawake kujikomboa kutoka katika makucha ya mila hii potofu.