Juhudi za dhati za wanawake
Mmoja kati ya wana-Blogi wa kiswahili (Bw. Ramadhani Msangi), katika makala yake moja ametamka maneno haya:- "Amka mwanamke wa Kitanzania, amka mwanamke wa Kiafrika. Popote pale ulipo katika dunia hii, amka SAA YA UKOMBOZI NI SASA". wakati akiuelezea mkutano wa kwanza na wa aina yake kuwahi kufanyika ambao utawahusu akina mama toka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine, nafasi na ushiriki wao katika ulimwengu wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano, kwa njia ya mtandao wa kompyuta.
Katika siku za karibuni, nitaendelea kuwataarifu zaidi juu ya kile kitakachokuwa kikiendelea wakati tukiuelekea mkutano huo unaokwenda kwa jina la Blogher utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu, nchini Marekani. Wakati tukiwa tunasubiri kujua kitakachotokea huko, wale ambao watahitaji kujua kuwa maandalizi yanakwenda vipi kwa lugha ya kingereza wanaweza pia kufuatilia kwa kusoma hapa.
Ni bahati nzuri pia kuwa huenda mambo yakiwa kama yanavyoandaliwa, atakuwepo au watakuwepo Watanzania watakaoshiriki mkutano huo kwa minajili ya kuuripoti kwa njia ya mtandao mkutano huo, katika lugha ya kiswahili. Fuatilia juu ya hili kwa kubonyeza hapa.