" Mafanikio daima ni kwa wale wenye Kujaribu bila kujali mara ngapi wanaanguka "

 

 

 
Wednesday, May 04, 2005

Mambo yanazidi kuiva, Ni kiswahili kwenda mbele sasa

Kiswahili, kiswahili kiswahili. Yaani ni kiswahili kwenda mbele hivi sasa. Hivi karibuni nimepokea na kupata anwani mpya za wanablogi wanaotumia lugha ya Kiswahili, ambazo ni pamoja na ya Martha Mtangoo na Beatrice Daffa, wanaoblogi kutokea Dodoma Tanzania na nyingine ya Indya Nkya, ambaye yeye yuko Moshi (Kilimanjaro) pia Tanzania.

Ndugu zangu, Watanzania wenzangu na wanablogi wenzangu, nina jambo moja ambalo napenda mlichukue kama neno langu la kuwakaribisha. Wakati nilipokuwa naanza kublogi kwa mara ya kwanza kabisa, sikuwa hata najua nini ninachokifanya, lakini kwa kadiri ambavyo nimekuwa nikiendelea nimekuwa nikibaini kuwa kumbe sikuwa napoteza muda wangu bure. Kuna mambo mengi ambayo yatakuja mbele yetu na hakika hatutajuta kupoteza muda wetu, kwa mujibu wa kaka yangu Ndesanjo. Karibuni wandugu wapendwa

1 Maoni ya Wasomaji:

Blogger Kishimba anasema...

Ndugu Ndesanjo;
Lugha ya Kiswahili ni kati ya lugha za Kiafrika ambayo inakua kwa haraka sana. Sababu mbalimbali (za kihistoria, kisiasa, kibiashara n.k.) zimechangia katika ufanisi huu. Wasiwasi wangu mkubwa ni hadhi hafifu ya lugha hii kwa watumiaji wake. Ni wazi kwamba Kiswahili hakina hadhi sawa na Kiingereza hata katika nchi ya Tanzania - nchi ambayo imejitwika jukumu la ulezi na u-mama wa lugha hii tamu. Wakati haya yakiendelea, Kiswahili, kama vile zimwi lisilo na huruma, kinameza lugha zingine za Kiafrika na kuna wasiwasi kwamba baada ya miaka 100 au 200 ijayo, lugha nyingi za Kitanzania zitakuwa zimeshakufa au zitakuwa mahututi. Swali ni kwamba, Kiswahili kweli kitakuwa na ubavu wa kusimama tisti na kupambana na Kiingereza? Isije ikawa Kiswahili kinajinenepesha kwa kumeza lugha zingine za Kiafrika na wakati huo huo kinajiandaa kuwa mlo mnono wa karne wa lugha ya Kiingereza.

N.B. Mimi ni profesa wa isimu ya kompyuta (computational linguistics) na lugha za kiafrika huku Marekani

6:25 PM  

Post a Comment

<< Rudi mwanzo

KUHUSU MIMI

JINA:Zainab Yusuph
MAKAZI:Dodoma
NCHI:Tanzania
KAZI:Mwandishi

BLOGI ZA KISWAHILI

 • Bangaiza
 • Mwandani
 • Pambazuko
 • Damija
 • Mtafiti
 • Martha
 • Gaphiz
 • Swahili time
 • Miruko
 • Dira yangu
 • Msangimdogo
 • Jeff Msangi
 • Kasri la mwanazuoni
 • Kurunzi
 • Baragumu
 • Mawazohuru
 • Fikra Thabiti
 • Mtandaoni
 • Motowaka
 • Mkwinda
 • Ngurumo
 • Nyembo
 • Bwaya
 • Omega
 • Tafakari za Maisha
 • Nuru akilini
 • Mtandawazi
 • Mhujumu
 • Vijimamboz
 • Wakati wa Ukombozi
 • Kijiwe Joto
 • Watoto Wetu
 • Jungu kuu
 • Kisima cha Weledi
 • Jarida la Ughaibuni
 • Bhalezee
 • Sauti ya Baragumu
 • Kona yangu
 • Furahia Maisha
 • Bakanja
 • Terrie Swai
 • Fatma Karama
 • Kazonta
 • Binti Afrika
 • Blogu ya Kilimo
 • Ukombozi
 • Mwafrika
 • Digital Africa
 • Blogu ya lugha mseto
 • BLOGI ZA WAAFRIKA

 • BLOGAFRICA
 • BLOGU ZA WAAFRIKA
 • DIGITAL AFRICA
 • MAMA JUNKYARD'S
 • MSHAIRI
 • KENYAN PUNDIT
 • MONGI DREAMS
 • ISARIA MWENDE
 • CUNNING LINGUISTICA
 • ETHIOPUNDIT
 • MOCHALICIOUS
 • UNGANISHA
 • DEMOKRASIA KENYA
 • CHANUKA
 • BANKELE
 • MAARIFA/AKIEY
 • AFROMUSING
 • NEHANDA DREAMS
 • BLACK LOOKS
 • YUMMY WAKAME
 • AFRICAN OIL POLITICS
 • NUBIAN SOUL
 • SANAA
 • VIRTUAL INSANITY
 • MENTAL ACROBATICS
 • KENYA UNLIMITED
 • JIKUMBUSHE KAZI ZANGU ZA ZAMANI

  2005-04 2005-05 2005-06 2005-07 2005-08 2005-11 2006-05 2006-06

  Imetengenezwa na

  Bonyeza hapa kumtembelea msangimdogo

  na inawezeshwa na